7 Dec 2010

Maji Matone yapokelewa kwa nyangwe wilayani Mbozi

Wapenda wote tunakumbuka ya kuwa Maji Matone tuliwasha mfumo wetu wa SMS tarehe 1/11/2010.

Tulianza kwa kurusha matangazo yetu katika radio tatu ambazo ni Uplands FM iliyopo Njombe, Abood FM iliyopo Mji kasoro bahari (Morogoro) na Mbeya Highlands FM iliyopo mkoani Mbeya.

Pia tulikuwa na warsha ya siku mbili ya kuwapa msasa wanahabari juu ya maradi, sera ya maji ya taifa pamoja na mambo lukuki juu ya uandishi wa habari zinazohusu maji na hali ya upatikanaji Tanzania vijijini.

Kiukweli nimepata faraja kubwa sana kwa huko Mbozi kwani mambo yalikuwa shwari. Hasa pale gari la la wanahabari lilipozungukwa na wananchi waliokuwa wakisoma machapisho ya Maji Matone huku wakihojiwa na wanahabari kwa ajili ya utayarishaji wa kipindi.

Jamani naomba nisimalize uhondo wote, tafadhalini angalieni baadhi ya picha nilizoweza kuzipata kutoka ripota wangu aliyeko Mbozi.

Tuongidze,
Fred
 
- - - -
Fred Kihwele,
Communications and Media Officer,
Maji Matone, Daraja.