8 Mar 2011

World Women's Day: Mwanamke wa Kijijini

From Casiana Ndimbo, Kwanza Jamii Njombe journalist

Mwanamke wa kijijini ni nguzo muhimu sana katika familia, yeye ndiye anayehusika kwa asilimia kubwa katika kusimamia mambo yote ya nyumbani ikiwa ni pamoja na kulea watoto, kupiki, kuhakikisha shughuli zote za nyumbani zinafanyika tena kwa wakati muafaka.

Mwanamke wa kijijini ni chachu ya mabadiliko ya kiuchumi na kijamii pia, tunaamini kuwa mwanamke anaweza kuleta mabadiliko makubwa sana katika jamii kwani wanawake wengi hupenda sana kufanya kazi mbailmbali ambazo zinawaingizia kipato.

Mwanamke wa kijijini bado anakabiliwa na mfumo dume, asilimia kubwa ya wanaume vijijini huwachukulia wananwake kama watumwa wa kazi za nyumbani na hawawezi kufanya jambo lolote la kimaendeleo kitu ambacho sio sahihi.

Mwanamke wa kijijini ni tofauti na mwanamke wa mjini ambaye kazi nyingi za ndani huweka mfanyakazi ambaye anazifanya kazi hizo badala yake, ndio maana anakuwa na muda mwingi wa kufanya kazi za kiuchumi na hivyo kujiongezea kipato.

Mwanamke wa kijijini huamka asubuhi na mapema kutafuta maji tena umbali mrefu sana akiwa na mtoto mgongoni, anatafuta kuni, anapikia familia na  hatimaye anajikuta siku nzima anaimaliza kwa kuihudumia familia tu bila kufanya mambo mengine ya kiuchumi,wakati huo  mwanamume yupo katika vilabu vya pombe.

Mwanamke wa kijijini anashindwa kujishughulisha na shughuli zingine za kiuchumi kutokana na kuzidiwa na kazi katika familia na hivyo kuwa tegemezi katika kaya.

Kuna shughuli ambazo mwanamke wa kijijini anazifanya hata mwanamume anaweza kuzifanya ili aweze kumsaidia mama huyu mwenye jukumu zito la kuilea famia, mfano kutafuta kuni, kuchota maji n.k, kazi hizi hata mwanamume anaweza kuzifanya ili aweze kuokoa muda ambao mwanamke angetumia.

Wanaume wakishirikiana na wake zao wataweza kuleta mabadiliko makubwa katika Nyanja ya kiuchumi.