15 Nov 2011

Proposed contents of Tanzania's Open Government Action Plan

As presented as a first draft to stakeholders consultation meeting by the Tanzania OGP Task Force, Nov 15, 2011. I will post a translation here later.

Uwazi:

 • Kuweka utaratibu wa kufanya madawti ya malalamiko yaliyoanzishwa ktk Wizara na Mamlaka za Serikali za Mitaa yafanye kazi
 • Kubaini na kuimarisha matumizi ya masanduku ya maoni yaliyopo ktk vituo vya kutolea huduma na kuweka utaratibu madhubuti wa kutambua yanavyofanya kazi
 • Kupitia upya majukumu ya Bodi na Kamati za Vituo vya utoaji wa huduma ktk sekta za afya, elimu na maji ili kuzifanya zitekeleze majukumu yake ipasavyo
 • Kuweka utaratibu ili kuhakikisha kuwa taarifa za mapato na matumizi zinabandikwa ktk mbao za matangazo ngazi za Halmashauri, kata, vijiji, mitaa na vituo vya kutolea huduma ktk sekta za elimu, afya, maji
Ushirikishwaji:
 • Kuweka taratibu madhubuti na rahisi za kufanya tovuti ya wananchi iweze kutumika kikamilifu
 • Kupitia upya mfumo wa O&OD ili uwe rahisi kutumika na wananchi na kuleta matokeo tarajiwa
 • Kupitia upya miongozo na taratibu za uendeshaji mikutano ya mashauriano na wadau juu ya ya upangaji mipango na bajeti ktk sekta za afya, elimu, maji, kwa lengo la kupata ushiriki mpana zaidi
Uwajibikaji na Uadilifu
 • Kuhusisha mikataba ya huduma kwa wateji (CSCs) ktk wizara na mamlaka za serikali za mitaa ili kuhakikisha yaliyomo yanatekelezwa
 • Kuimarisha taratibu zilizopo za ufuatiliaji wa mapato na matumizi ya fedha za umma (PETS) kwa lengo la kubaini thamani ya fedha
 • Kuhusisha vigezo vya utoaji wa ruzuku ya matumizi ya kawaida na maendeleo ktk halmashauri
 • Kuweka taratibu madhubuti za kusimamia mapato na matumizi ya fedha kwa kutumia Integrated Financial Management System (IFMS) ambayo imewekwa ktk mikoa, wizara na halmashauri zote
Teknolojia na Uvumbuzi
 • Kuandaa ramani zinazo vituo vya utoaji maji nchini ili taarifa hizo zitumike kupanga mipango endelevu ya maji. Utaratibu huu unatusaidia wananchi kutoa taarifa kwa viongozi wao kuhusu ufanyaji kazi wa vituo vya maji vilivyopo
 • Kuongeza kasi ya matumizi ya TEHAMA ktk kuongeza ufanisi wa kufundisha na kujifunzia
 • Kuhakikisha teknolojia ya matibabu kwa njia ya masafa (telemedicine) inatekelezwa kama ilivyotarajiwa.
 • Kutoa taarifa mbalimbali za utoaji wa huduma (elimu, afya, maji) kwa wananchi kwa kutumia njia za teknolojia ya habari na mawasiliano kama vile tovuti, simu za mikononi, televisheni, kompyuta, redio na sms.